WASHAMBULIAJI  wa Simba, Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo wameipa pointi tatu leo timu yao baada ya mabao yao kuwafanya watoke uwanjani kifua mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwneye Uwanja wa Uhuru.
 Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao. Kocha Omog aliamua kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake ambapo mabadilikoa hayo yalionekana kubadili kasi ya mchezo kabla ya Ajib kuandika bao la kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona iliyopigwa na Kichuya dakika ya 52.
Mavugo alifunga bao la pili kwa shuti dakika ya 66 pasi kutoka kwa Kazimoto. Baada ya bao hilo kuingia SImba waliendelea kutafuta mabao mengine kwa kasi ambapo straika wake Muivory Coast Blagnon almanusura afunge bao la tatu lakini mpira wake uliokolewa na kipa wa Mtibwa .

Post a Comment

 
Top