Juuko

KATIKA hali isiyotarajiwa, beki wa kati wa Simba, Juuko Murshid bado hajajiunga na wenzake tangu alipoondoka kikosini hapo katikati ya wiki iliyopita alipokwenda kuitumikia timu yake ya taifa.

Juuko ambaye msimu huu tangu uanze ameonekana hana nafasi ndani ya Simba, alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda kilichoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Comoro, na kutinga michuano ya mataifa Afrika (Afcon).

Mganda huyo alitakiwa kujiunga na wenzake tangu Jumanne ya wiki hii, lakini hakufanya hivyo huku akitafutwa kwa njia mbalimbali ikiwemo simu, lakini hakupatikana.

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, ameliambia gazeti hili kuwa: “Juuko hajafika na sina taarifa zake kwa nini hajajiunga na timu kwa sababu alitakiwa awe hapa mara tu alipomaliza majukumu ya timu yake ya taifa kama walivyofanya wenzake.


“Lakini ukiangalia kwenye kikosi chao cha Uganda, wachezaji wote wamejiunga na klabu zao, kasoro yeye. Nilimwambia Mayanja (Jackson kocha msaidizi wa Simba) naye amtafute, lakini hakumpata, sasa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha lazima nimuadhibu.

“Nitauambia uongozi umkate mshahara wake wa mwezi huu ili kumkumbusha kwamba ni lazima awe na nidhamu ndani ya kikosi changu.”

Post a Comment

 
Top