Mechi mbili
za raundi ya sita za Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Majimaji, na African
Lyon na Kagera Sugar sasa zitachezwa kwenye Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa
Uhuru.
Mabadiliko
hayo yametokana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusitisha kwa
muda kuutumia Uwanja wa Uhuru katika kipindi hiki ambacho limeanza kufanyia
marekebisho sehemu ya uwanja huo ambayo ni ya nyasi bandia (artificial turf).
Hivyo, mechi
ya Simba na Majimaji itafanyika Jumamosi, Septemba 24 wakati ile ya African
Lyon na Kagera Sugar itachezwa Jumatatu, Septemba 26. Jumapili, Septemba 25
Uwanja Taifa utatumiwa kwa mechi ya timu za Wabunge za Simba na Yanga ili
kuchangia waathirika wa janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
kikosi cha Lyon |
Mechi
nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa Jumamosi, Septemba 24 ni kati ya
JKT Ruvu na Mbeya City (Mabatini), Ndanda na Azam (Nangwanda Sijaona), Tanzania
Prisons na Mwadui (Sokoine), Mtibwa Sugar na Mbao (Manungu).
Jumapili
kutakuwa na mechi kati ya Stand United na Yanga (Kambarage), na Ruvu Shooting
na Toto Africans kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.
Kutokana na
marekebisho yanayofanyika Uwanja wa Uhuru, mechi ya kundi ya A ya Ligi Daraja
la Kwanza kati ya Ashanti United na Pamba iliyokuwa ichezwe Ijumaa, Septemba 23
kwenye uwanja huo sasa itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini
Dar es Salaam.
Post a Comment