KOCHA Mkuu wa
Yanga, Mholanzi, Hans Pluijm, ameziambia timu pinzani kuwa ziendelee kuipania
timu yake lakini zijue kuwa lazima zikumbane na kichapo tu mbele ya Yanga.
Kauli hiyo
aliitoa mara baada ya mechi dhidi ya Mwadui FC inayofundishwa na kocha, Jamhuri
Kihwelo 'Julio' iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa
Kambarage, Shinyanga.
Yanga hivi
sasa imefikisha pointi 10 sawa na Azam FC iliyofungwa na Simba, juzi lakini
Jangwani wapo nafasi ya pili wakiwa na uwiano mzuri zaidi wa mabao. Simba ndiyo
inayoongoza ligi baada ya ushindi wa juzi.
Pluijm alisema
hivi sasa anaingia uwanjani na tahadhari kwa lengo la kupata ushindi kutokana
na kila timu anayokutana nayo kucheza kwa kuwapania kwa lengo na kutaka
kuifunga Yanga.
Pluijm alisema
yeye atakachokifanya hivi sasa katika mechi zake za ligi, ni kutoidharau timu
yoyote na badala yake atapanga kikosi kitakachompa ushindi kuhakikisha anakaa
kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu.
“Ujue hivi
sasa kila timu inayokutana nasi inacheza kwa kutupania kwa maana ya kucheza kwa
kujihami kwa kulinda goli lao huku wakicheza rafu za makusudi.
"Lengo
lao ni kutaka kutufunga ili waweke historia, hivyo nimeliona hilo na nimepanga
kulidhibiti kwa kukiandaa kikosi changu vema ili kuhakikisha tunawafunga mwisho
wa mchezo.
"Lakini napenda
nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji wangu kwa kucheza kwa kujituma kwenye
mechi zetu nne tulizozicheza ambazo tatu tumeshinda na nyingine moja tumetoka
sare na Ndanda FC,” alisema Pluijm.
Juzi, Yanga
iliichapa Mwadui mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kwa mabao ya
Amissi Tambwe na Donald Ngoma.
Post a Comment