JUUKO
Murshid, juzi jioni alitua Bongo kwa ajili ya kuanza kuitumikia Simba lakini kauli
aliyoitoa Rais wa Simba, Evans Aveva hivi karibuni, moja kwa moja inamfanya
kocha wa kikosi hicho, Joseph Omog kumpa nafasi ya kucheza kikosini kwake beki huyo
mahiri raia wa Uganda.
Murshid
aliipa presha kubwa Simba, kwani tangu aende kuitumikia timu ya taifa ya Uganda,
wiki moja iliyopita hakurejea hadi juzi huku siku zake zikiwa hazipatikani.
Ilielezwa kwamba amefanya mgomo baridi kutokana na kukerwa kuwekwa benchi na
kocha Joseph Omog. Tayari ameambiwa aandike barua ya kujieleza.
Lakini
Aveva amesema anataka kuona wachezaji wote wa kimataifa waliopo ndani ya Simba
wanapata nafasi ya kucheza kwani ni moja ya makubaliano yao na benchi hilo la
ufundi linaloongozwa na Omog.
Tangu
msimu huu uanze, Juuko amekosa nafasi ya kucheza kikosini hapo huku nafasi
anayoicheza ya beki wa kati ikichezwa na Method Mwanjali na Novaty Lufunga.
Ikumbukwe
msimu uliopita, Juuko alitengeneza ukuta imara kikosini hapo kiasi kwamba
alikuwa ndiyo tegemeo na alipokosekana basi Simba ilikuwa na wakati mgumu,
lakini msimu huu imekuwa tofauti.
Taarifa
za uhakika kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, zinasema Aveva
amekuwa akishangaa kuona Juuko hajapewa nafasi mpaka sasa wakati anaamini uwezo
bado anao wa kuitumikia Simba kama ilivyokuwa msimu uliopita.
“Unajua
hakuna anayeamini kama Juuko sasa hivi hana nafasi kikosini, hata rais Aveva
naye anashangaa hilo wakati awali walikubaliana na Omog na kumhakikishia kwamba
profesheno wote lazima awape nafasi, lakini utaona mpaka sasa kama vile dalili
hizo hakuna.
“Wakati
wa kipindi cha usajili Omog aliambiwa achague wachezaji ambao anaona watakuwa
msaada kikosini isije kutokea kama huko nyuma kujaza wachezaji halafu hawana
nafasi, kwani hatutaki kuona tunarudi kule tulipotoka. Kitendo cha Juuko
kuwekwa benchi kinamshangaza Aveva na sasa anataka aone akichezeshwa,” alisema
mtu huyo.
Hivi
karibuni, Omog alisema Juuko bado ana nafasi ya kucheza kikosini hapo na kwa
sasa anampumzisha mpaka pale ligi itakapochanganya kwani aina ya uchezaji wa
Juuko ni wa nguvu, hivyo anamuandaa kuja kupambana na timu ngumu ambazo ndiyo
levo ya beki huyo.
Post a Comment