KATIKA kuelekea mechi dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Simba,
Mcameroon, Joseph Omog, amesema anataka kuona washambuliaji wake wanatumia kila
nafasi watakayoipata ndani na nje ya 18.
Timu hizo kongwe, zinatarajiwa kuvaana Oktoba Mosi, mwaka
huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Mrundi, Laudit
Mavugo, Ibrahim Ajib, Frederick Blagnon huku wakisaidiwa na kiungo
mshambuliaji, Shiza Kichuya.
Omog |
Omog alisema tayari ameshawaambia wachezaji wake katika
hilo, kikubwa anataka kuona timu hiyo inatoka uwanjani ikiwa na ushindi wa aina
yoyote.
Omog amesema tayari amewapa mbinu mbalimbali za ufungaji
wa mabao kwa njia ya mashuti nje na ndani ya 18, kumchambua kipa na kutumia
vema mipira ya krosi na kona kwa ajili ya kupiga vichwa.
“Nitakuwa mkali kwa yule mshambuliaji atakayeleta
masihara ya kushindwa kutumia kila nafasi tutakayoipata ndani ya uwanja kwa
ajili ya kufunga mabao.
“Kama unavyojua, siku zote bahati haiji mara mbili, hivyo
basi ni vema washambuliaji wangu wakaongeza umakini kwa kuitumia vema kila
nafasi tutakayoipata tutakapokutana na Simba na timu nyingine zinazoshiriki
ligi kuu.
“Kikubwa nitaka niendelee kukaa kileleni hadi mwisho mwa
ligi kuu ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa wa ligi kuu, ninavyojua siyo
kazi rahisi, lakini tutapambana ili tufanikishe malengo yetu,” alisema Omog.
Post a Comment