BEKI
wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Boniface Pawasa, ameangalia mfumo unaotumiwa
na Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, kisha akasema kama kweli anataka wafunge
mabao mengi, basi ni lazima aubadilishe.
Pawasa
amekosoa mfumo huo wa Omog wa kuwapanga pamoja washambuliaji Laudit Mavugo na
Ibrahim Ajib kwa wakati mmoja huku akisema washambuliaji hao wanacheza soka la
kufanana.
“Ukiangalia
uchezaji wa Mavugo ni kama namba kumi, pia Ajib anacheza kama hivyo, yaani wote
wakiwa katika kikosi cha kwanza utaona anakosekana mshambuliaji wa mwisho
ambaye muda wote anatakiwa kuwa kwenye eneo la hatari la wapinzani.
“Kwa
mfumo anaoutumia Omog, hana budi kuwachezesha Ajib na yule Muivory Coast
(Frederic Blagnon) au Mavugo na huyo jamaa (Blagnon) kwani yeye nimemuona ndiye
anaweza kucheza kama mshambuliaji wa mwisho tofauti na hao wengine.
“Kama
Omog akiendelea kuwatumia zaidi Ajib na Mavugo kwa pamoja, basi watakuwa na
kazi kubwa ya kufanya kwenye kusaka ushindi, wanaweza kushinda lakini si
kirahisi,” alisema Pawasa.
Post a Comment