FAINALI ya michuano ya Mobisol Cup inatarajiwa kupigwa kesho Jumapili kwenye
Uwanja wa Sokoine uliopo mkoani hapa kwa timu za Mbeya City U-20dhidi ya
Zaragoza ambapo kiingilio ni bure.
Mratibu wa
mashindano hayo, Jirani Mtembezi, amesema maandalizi kuelekea mchezo huo
yamekamilika na kabla ya mchezo huo kutakuwa na mchezo wa utangulizi kati ya
mashabiki wa Simba na Yanga.
"Maandalizi
ya mchezo huo yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda ufike ili tujue bingwa
mpya wa mashindano haya ni nani. Tunawashukuru Wana-mbeya kwa kuungana nasi
tangu mashindano haya yameanza mpaka yanaelekea kufikia tamati Jumapili hii.
“Kikubwa ninaomba
mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kushangilia timu zao na kwa zile timu ambazo
zilitolewa mapema ni vyema nazo zikaja kusapoti kwenye mechi hii ya fainali
inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa,” alisema Jirani Mtembezi.
Bingwa wa
mashindano hayo ataondoka na fedha taslimu Sh milioni tatu, wa pili
atajinyakulia milioni moja na wa tatu Sh 500,000 wakati mfungaji ni Sh 100,000.
Post a Comment