WACHEZAJI WA SIMBA WAKISHANGILIA MOJA YA MABAO WALIYOFUNGA MSIMU HUU

UPINZANI wa mechi ya Simba na Yanga una faida yake ambapo kulingana na ukubwa wa mechi hiyo, vigogo wa Simba wameamua kuwaongezea dau la ‘bonus’ wachezaji wao wanalowapa katika mechi nyingine, pale wanapofanikiwa kuibuka na ushindi.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Simba imejiwekea utamaduni wa kuwapa wachezaji shilingi milioni tano kila timu hiyo inapoibuka na ushindi lakini katika mechi dhidi ya Yanga, dau hilo limeongezeka maradufu.

Mmoja wa vigogo wa timu hiyo amelitonya Championi Ijumaa kuwa, makubaliano ni kwamba kama Simba itaibuka na ushindi katika mechi hiyo, basi dau hilo la milioni tano watalipata mara mbili zaidi na kwamba mwanachama mwingine mwenye ushawishi mkubwa klabuni hapo naye ametoa ofa kuwa bonus yoyote watakayopewa vijana hao baada ya mechi hiyo basi na yeye ataitoa ileile kutoka mfukoni mwake.
BENCHI LA UFUNDI LA SIMBA
“Hii ni mechi kubwa, hata bonus imeongezeka, itakuwa mara mbili zaidi ya ile ya kawaida au zaidi ya hapo, lakini haiwezi kushuka na kwamba (anamtaja jina) naye amejitolea kwamba kiasi watakachopewa vijana siku hiyo na uongozi basi na yeye atatoa kingine kama hicho kwa ajili ya kuwaongezea zaidi,” alisema kigogo huyo.

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi nchini kote, inatarajiwa kupigwa Oktoba Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Post a Comment

 
Top