LICHA ya kufanya vuema uwanjani na kufikia hatua ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la FA na kufanikiwa kushiriki Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, Yanga bado inaonekana kuifunika timu ambayo ni watani wao, Simba hata nje ya uwanjai, hiyo ni kupitia malipo ya mishahara.
Wachezaji wanaolipwa zaidi kwa upande wa Yanga wamefungana watatu ambao ni Donald Ngoma, Chirwa, Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima ambao wanakomba kitita cha dola 3,500 kila mmoja (zaidi ya Sh milioni saba) kwa mwezi.
Kwa upande wa Simba mchezaji anayelipwa zaidi ni Blagnon na Laudit Mavugo raia wa Burundi ambao wamefungana kwa kulipwa dola 1,500 (zaidi ya Sh milioni tatu) kwa mwezi.
Ukilinganisha hapo utakuta Simba imepotezwa tena, kwani wachezaji wao wanaolipwa zaidi wapo chini kwa kiasi cha Sh milioni nne ukilinganisha na wale wa Yanga.

Post a Comment

 
Top