Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ametoa ofa kwa
wananchi kujumuika pamoja leo Septemba 18, 2016 katika mchezo wa mpira wa miguu
utakaozikutanisha timu za vijana taifa za Tanzania na Congo-Brazzaville kwenye
Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.
Timu hizo
zitakutana kweye mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka. Zinatarajiwa
kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itafayopata ushindi wa
jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo.
Nape alitoa
ofa hiyo tangu jana Septemba 17, 2016 na leo asubuhi Septemba alipata kifungua
kinywa na wachezaji wa Serengeti Boys ambako alitoa Sh 200,000 kwa kila
mchezaji zilizotokana na kundi linalosapoti Serengeti Boys ambao walichangia Sh
2,600,000 wakati nyingine zilitoka kwa wadau wengine.
Nape
ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha hizo kadiri ya
idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake itakuwa Sh 5,000,000.
“Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa fedha zaidi, kwa hiyo
Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo mbele ya Watanzania watakaoingia
uwanjani bure.”
Kuingia bure
kesho ni ofa iliyotolewa na Nape ambako Rais Jamal Malinzi amemshukuru Nnauye
ambaye ni Mbunge wa Mtama kwa ofa hiyo ambayo imelenga kutoa hamasa kwa
Watanzania kwenda kushangilia timu yao.
Katika
mchezo huo ambao Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, amesema kwamba amemaliza kila
kitu na kwamba anasubiri Watanzania kuja uwanjani leo kuishangilia timu yao,
utachezwa na waamuzi kutoka Shelisheli ambako mpiga kipenga atakuwa Nelson Fred
akisaidiwa na Hensley Petrousse na Stive Marie wakati mwamuzi wa akiba akiwa
Allister Barra. Kamishna wa mchezo atakuwa Gladmore Muzambi kutoka Zimbawe.
Post a Comment