BAADA ya Simba kuibuka na
ushindi wa pili katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara, vigogo wa timu hiyo
wameamua kuwamwagia noti wachezaji hao ikiwa kama pongezi ya ushindi wao huo.
Simba ilifanikiwa kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo huo uliopigwa juzi
kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar lakini dakika chache baada ya kumalizika kwa mchezo
huo, wachezaji hao wakapewa zawadi hiyo ya kitita cha shilingi milioni tano.
Mmoja wa watu wa ndani wa
timu hiyo, amesema fedha hizo walitengewa tangu walipocheza mechi yao ya pili
ya ligi dhidi ya JKT Ruvu, lakini kwa kuwa hawakuibuka na ushindi, hawakupewa
chochote mpaka walipoifunga Ruvu.
“Hizo fedha zilikuwepo tangu
awali, wenyewe tu kwa kuwa hawakufanya vizuri katika mechi na JKT ndiyo maana
hawakuambulia kitu lakini imekuwa safi wameshinda katika mchezo na Ruvu
Shooting, ndiyo maana wamepewa zawadi yao na itagawanywa kulingana na mchango
wa kila mchezaji, aliyeanza ‘first eleven’, aliyekaa benchi mpaka jukwaani,”
alisema kigogo huyo.



Post a Comment