WAKATI kesho Jumamosi straika wa
Simba, Mrundi, Laudit Mavugo akitarajia kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba
kuwavaa Azam FC, mshambuliaji huyo ameweka bayana alichokutana nacho kwenye
mechi nne za Ligi Kuu Bara mpaka sasa.
Mavugo aliyeifungia Simba
mabao matatu kwenye mechi nne, ametamka kwamba ushindani wa ligi hiyo ni mkubwa
zaidi ya aliokuwa anakutana nao nchini kwao Burundi,ambapo mabeki wengi
wamekuwa wakicheza zaidi ya kazi ili kulinda timu yao isifungwe.
Straika huyo wa
zamani wa Vital’O ya Burundi amesema, kwamba wapinzani wao hasa mabeki,
wamekuwa wakiwafanyia vitendo visivyo vya kimichezo ili kuwaondoa katika hali
ya kimchezo na pia wasipate nafasi ya kufunga bao.
“Bongo mambo ni magumu kwa
sababu wapinzani mara nyingi wanatufanyia
vitendo ambavyo ni vya kukera na visivyo vya kimpira kwa lengo tu watuondoe
katika hali ya kiuchezaji lakini pia hiyo ikiwa ni mbinu ya wao kujilinda.
“Lakini kwangu wala
sijali na badala yake nitaendelea kupambana zaidi na zaidi kuitetea timu yangu kuhakikisha
inaibuka na ushindi katika kila pambano,” alisema Mavugo.
Post a Comment