USIKU wa leo Jumatano, Septemba 28,
macho na masikio ya wapenda soka ulimwenguni kote yataelekezwa jijini Madrid,
nchini Hispania, katika dimba la Vicente Calderon, uliopo Wilaya ya Arganzuela.
Kwa mujibu wa vipimo, Vicente
Calderon ni uwanja unaotajwa kuwa ni mkubwa katika sehemu ya kuchezea, ukiwa na
urefu wa mita 105 na upana mita 70. Ni mkubwa kuliko viwanja maarufu kama
Allianz Arena, Old Trafford, Nou Camp, Anfield na hata Santiago Bernabeu.
Usiku wa leo, nyasi za uwanja huo
zitawaka moto, wakati miili ya wanaume 22 itakapokuwa inapambana katika mechi
inayochukuliwa kuwa itakuwa yenye kusisimua mno.
NI MECHI YA KULIPA KISASI?
Timu yoyote itakayoibuka mshindi
usiku wa leo kati ya Atletico au Bayern Munich itakuwa imelipa kisasi kwa namna
fulani.
Carlo Ancelotti na Diego Simeone wamekutana mara 13 ndani ya miaka mitatu iliyopita, huku Diego Simeone akiibuka na ushindi katika mechi tano, wakati mechi nne akipoteza dhidi ya Carlo Ancelotti na mechi nne wakitoshana nguvu.

Carlo Ancelotti aliweza kumfunga
Diego Simeone katika michuano ya Copa del Rey hatua ya nusu fainali, akiibuka
mshindi nyumbani na ugenini katika msimu wa 2013/2014. Pia Carlo Ancelotti aliibuka
mshindi katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kule Lisbon -Ureno.
Vile vile aliweza kumwondoa Diego
Simeone msimu wa 2014/2015 katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya kwa goli la ‘Chicharito’, baada ya kutoa sare katika mechi ya kwanza.
Hata hivyo, Ancelotti hakuwahi kumfunga Diego Simeone katika mechi yoyote ya La
Liga, mpaka anatimuliwa Real Madrid mwaka 2015.
Ni msimu uliopita tu wakati Diego
Simeone alipoweza kuiongoza Atletico Madrid kuiondoa Bayern Munich, iliyokuwa chini
ya Pep Guardiola katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa hiyo, mechi hii ya hatua ya makundi inaweza kuchukuliwa kama kisasi kwa makocha wote wawili. Ushindi wa Bayern dhidi ya Atletico utakuwa na maana kubwa kwao na kocha wake, Ancelotti kwa sababu ya kuonekana ana takwimu mbovu dhidi ya Diego Simeone wanapokutana.
Na ushindi wa Atletico Madrid utakuwa na maana nyingine ya kuendeleza ubabe wake kwa Bayern na pia kulipa kisasi kwa Carlo Ancelotti kwa kipigo walichokipata mara ya mwisho Aprili 22, 2015, wakati huo Ancelotti akiwa kocha wa Real Madrid.

ANTOINE GRIEZMANN VS ROBERT
LEWANDOWSKI
Mioyo ya mashabiki wa kila timu
usiku huu itaelekezwa kwa watu hawa wawili. Wanaume hawa wawili wameibuka kuwa
washambuliaji hatari mno msimu huu, mpaka sasa Antoine Griezmann akiwa amefunga
magoli 5 katika mechi 6 alizocheza kwa mashindano yote, wakati mpinzani wake,
Robert Lewandowski akiwa ameshatupia magoli 6 katika mechi 6 za mashindano yote
msimu huu. Kosa moja la mabeki wanaweza kukuadhibu.
VITA YA SEHEMU YA KIUNGO.
Sifa kubwa ya Atletico ni kuwa na
wachezaji wengi mahiri na wenye nguvu katika sehemu ya kiungo. Kama uliweza
kuwatazama vyema katika mechi yao ya sare dhidi ya Barcelona, unaweza
kukubaliana nami. Katika mfumo wa 4-2-3-1 anaopenda kuutumia Diego Simeone mara
nyingi umepelekea kutawala sana sehemu ya kiungo.
Hata hivyo, usiku wa leo Atletico
Madrid inakutana na Bayern Munich mpya kabisa. Carlo Ancelotti ni muumini wa
mfumo wa 4-3-3, akitumia sana viungo watatu madhubuti kati.
Kazi kubwa leo itakuwa kati ya Yannick Carrasco, Saul Niguez, Koke, Nico Gaitan, Angel Correa dhidi ya wale wa Bayern akina Alonso, Artulo Vidal, Joshua Kimmich, Thiago Acantara, Renato Sanchez na Frank Ribery. Hakika ni jasho na damu usiku huu.

HAWA WATAKOSEKANA
Atletico Madrid watawakosa wachezaji
wake wawili muhimu mno usiku huu, akiwemo kiungo wake bora, Augusto Fernandez,
pia itawakosa beki wake Jose Gimenez, kiungo mkongwe Tiago Mendez, Alessio
Cerci na kipa wake, Angel Moya, walio majeruhi.
Bayern Munich wao hawatakuwa na
pengo kubwa pamoja na kuwakosa Douglas Costa na Holgar Badstuber, huku kukiwa
na hatihati kumkosa beki wake mahiri, Mats Hummels, walio majeruhi.
TIMU IPI ITAIBUKA NA USHINDI?
Kiwango cha Bayern Munich msimu huu
kinatisha. Wamecheza mechi sita na kushinda zote. Chini ya Carlo Ancelotti
Bayern taratibu wanaanza kurejea katika aina ya asili ya soka lao la kasi na
pasi ndefu za haraka haraka.
Ni wazuri pia kwa mipira ya
kushtukiza, huku wakiwa na wachezaji wenye uwezo wa kupiga mashuti hata nje ya
18. Ni hatari zaidi kwa mipira ya kona na krosi.
Msimu huu wameimarika mno, tofauti
na msimu uliopita. Kurejea kikosi cha kwanza kwa Javi Martinez na kuwasili kwa
Mats Hummels na Renato Sanchez na kuibuka kwa kinda Joshua Kimmich kumewafanya
Bayern Munich wawe imara zaidi kuliko msimu uliopita.
Atletico Madrid hawajaanza vyema
msimu huu wakiwa wamecheza mechi saba, huku wakitoa sare mechi mbili na
kushinda tano. Msimu huu Atletico Madrid ni moja ya timu zilizofanya vyema
katika dirisha la usajili kwa kuwatwaa wachezaji bora na mahiri kama Nico
Gaitan na Kelvin Gameiro.
Ni imara sana katika sehemu ya
kiungo na ushambuliaji, huku sehemu ya ulinzi nako kukiwa na wanaume wa shoka
kweli kweli. Atletico Madrid wakiwa nyumbani kwao Vicente Calderon wanakuwa timu
tofauti. Ni ngumu mno kuwafunga nyumbani kwao.
Mshindi wa mechi hii atakuwa
amejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa na nafasi kubwa ya kuongoza kundi hili
‘D’ kwa hatua inayofuata. Ni mechi kubwa na bora kuitazama usiku huu.
MAKALA: DIMBA
Post a Comment