Tambwe na Kocha Pluijm
OKTOBA mwaka 2013 ni mwezi ambao Mrisho Ngassa hataweza kuusahau kutokana na ahadi yake kuhusu mechi ya Simba na Yanga, sasa Amissi Tambwe amesema hataki kufanya mzaha.
Ngassa ambaye sasa amesajiliwa na Fanja FC ya Oman, wakati huo (2013) alikuwa akiichezea Yanga na ilipokaribia mechi dhidi ya Simba, akaweka nadhiri ya kusema asipofunga bao nyumba zake zichomwe moto.
Ikumbukwe ya kuwa, Ngassa ana nyumba zisizopungua tano ambazo tatu zipo Mwanza na mbili zipo Dar es Salaam.
Kwa bahati nzuri Ngassa alifunga bao moja katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuisha kwa sare ya mabao 3-3.

Ngassa
Straika wa Yanga, Tambwe ambaye ana mabao matatu sasa kwenye ligi yeye alisema: “Ngassa alikuwa anajiamini sana, ila mimi sitaki kuweka ahadi ya kuharibu kitu changu.
“Lakini nakuhakikishia lazima niwafunge Simba na ikishindikana hata pasi ya bao nitatoa lakini kubwa zaidi ni kuwa tuna uhakika wa kushinda mechi dhidi yao.”
Simba na Yanga zitacheza Oktoba Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa na Tambwe raia wa Burundi atacheza mechi hiyo akiwa na kumbukumbu ya kuifunga timu hiyo mara mbili katika mechi mbili msimu uliopita.

Post a Comment

 
Top