MAHADHI |
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kesho Jumamosi
Septemba 24, 2016 itasikiliza mashauri 13.
Malalamiko hayo ni:
1. Mchezaji Ametre
Richard ambaye atawasilisha mbele ya kamati makubaliano waliyokubaliana kukaa
pamoja na kufikia mafaka.
2. Klabu ya Coastal
Union dhidi ya Simba kuhusu madai ya fidia kwa wachezaji Hamad Juma na Abdi
Banda.
3. Ally Rashid Ally
dhidi ya Simba, malalamiko ya kunyimwa stahiki zake
4. Mchezaji Abdallah
Juma dhidi ya Mbeya City, madai ya malimbikizo ya mshahara, fedha za usajili na
gharama za matibabu.
5. Simba dhidi ya
Young Africans, madai ni kuingia mkataba na mchezaji Hassan Kessy wakati ana
mkataba na Klabu ya Simba
6. Kocha Abdul H.
Banyai, kesi ni madai ya stahiki zake.
7. Coastal dhidi ya
Young Africans, madai ya fidia ya matunzo ya mchezaji Juma Mahadhi
8. Saleh Malande
dhidi ya Ndanda FC madai ya uvunjikaji wa mkataba
9. Coastal Union
dhidi ya Mbeya City, madai ya fidia ya fidia kwa matunzo ya mchaji wao.
10. Sputanza FC dhidi ya Mbeya City, madai ya ada na usajili
na mishahara
11. Kimondo FC dhidi ya Ruvu JKT, majibu ya kumalizana kati
ya timu hizo mbili
12. Mathias Lule dhidi ya Stand United, taarifa ya kushindwa
kufikia makubaliano ya kulipana.
13. Kimara United FC dhidi ya Kurugenzi FC, pingamizi la
mchezaji Martine Sepeni kusajili timu ya Kurugenzi ya Iringa.
Post a Comment