Wanandoa
wenye jina kubwa kwenye ulimwengu wa filamu duniani, Bradd Pitt na Angelina
Jolie, wameachana.
Jolie
amesaini nyaraka za talaka ya kuachana na mume wake Brad Pitt akidai kuwa
wameshindwa kutatua tofauti zao.
Nyaraka za
mahakama zinaonyesha kuwa wanandoa hao waliachana rasmi Septemba 15 ikiwa ni
miaka miwili na mwezi mmoja tangu waoane mnamo Agosti 2014.
Kwa sasa,
Jolie anatafuta ulezi wa watoto wao sita na ameitaka mahakama imruhusu Pitt
kuwatembelea watoto wao.
Pitt
alisema: “Nimeumizwa sana na hili ninachoangalia ni watoto sasa hivi.”
Naye wakili
wa Jolie, Robert Offer alisema uamuzi wa talaka umefanywa kwa ajili ya familia.
“Jolie
hawezi kuzungumza chochote kwa sasa na ameitaka familia hiyo iachwe katika
wakati huu mgumu.”
Post a Comment