WAKATI Simba wakienda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kupeleka ushahidi wa aliyekuwa beki wao, Hassan Kessy kuusitisha mkataba wake
na timu hiyo, mwenyewe amepanga kuongeza program ya mazoezi binafsi ya gym.
Suala la Kessy, hivi karibuni lilichukua sura mpya baada
ya kuanza kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF huku
ikijumuisha viongozi wa Yanga kwa ajili ya utetezi.
Wakati suala hilo likiendelea, beki huyo tayari
ameruhusiwa na TFF kuanza kuitumikia Yanga inayonolewa na Mholanzi, Hans van Pluijm
akiwa ameshacheza mechi tatu za timu hiyo.
Kessy alisema amepanga kujitenga na kufanya mazoezi ya
kuongeza fiziki na fitinesi katika kujiweka fiti zaidi ya alivyo hivi sasa.
“Kama unavyojua hadi kufikia suala hili linamalizika na
mimi kuruhusiwa na TFF kuichezea Yanga, mengi yalitokea lakini nashukuru
yameisha, hivyo nimepanga kuingia gym kwa ajili ya kuongeza ufiti.
"Ninataka niwe na stamina, kasi na pumzi za kutosha
katika kupeleka mashambulizi kwenye lango la timu pinzani, hivyo ni lazima niwe
fiti kuhakikisha ninaendana na kasi hiyo, gym ndiyo suluhisho la hilo," alisema
Kessy.
Post a Comment