Muandaaji wa
shindano hilo, Flora akiwa katika pozi
|
MSHINDI wa shindano la Ozona Miss Lake
Zone anatarajiwa kuondoka na gari aina ya Toyota Passo yenye thamani ya Sh
Milioni 12.5.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika
Septemba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Rock City Mall, ambapo warembo 18
kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa watakuwa jukwaani kuwania taji hilo.
Mfano wa
gari atakalopewa mshindi
|
Mwandaaji wa shindano hilo, Flora Lauo,
alisema kila kitu kimakamilika kuelekea kwenye shindano hilo na kwamba
washiriki wote wapo tayari na wanatarajiwa kuleta ushindani mkubwa kutokana na
maandlizi yao ya nguvu.
Mbali na gari, pia kutakuwa na zawadi
nyingine mbalimbali kutoka kwa wadhamini wa shindano hilo ambao ni Ozona, Grace
Product, Halotel, KK Link Home Security, Tecno, Windhoek, Nyanza Bolting Ltd,
Nitetee Foundation, Chief Phones & Accessories.
Post a Comment