Kamati ya
Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iimeahirisha kikao chake kilichokuwa kikae
kesho Jumapili Septemba 4, 2016 kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan
Ramadhan Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya
mazoezi na klabu ya Young Africans sambamba na kusajili katika timu hiyo ya
Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho Juni 15,
2016.
Simba
imelalamika mbele ya kamati hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kuwa, mchezaji Hassan Kessy alivunja taratibu hizo akiwa ndani ya mkataba wa
klabu hiyo yenye mashakani yake Barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu
wa taarifa ya Kamati hiyo, shauri hilo lilisikilizwa baadaye mwezi huu katika
tarehe itakayopangwa hapo baadaye. Sababu za kuahirisha kikao hicho ni
kutotimia kwa idadi ya wajumbe wa kamati nzima. Ni lazima wajumbe zaidi ya
watatu wathibitishe kushiriki.
Ilikuwa isikiliwe kesho baada ya kushindikana
kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu Klabu Simba ikiilalamikia Klabu Young
Africans, kuingia mkataba na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy wakati bado ana
mkataba na klabu Simba.
Shauri la
Simba dhidi ya Young Africans lilishindika kusikilizwa kwa sababu Young
Africans hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo,
hivyo kamati itaiandikia barua Young Africans kukumbushwa kuhudhuria kwenye
kesi hiyo Jumapili ijayo kabla ya kutolewa uamuzi.
Kama
hawakutokea tena, shauri hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi
upande mmoja. Kadhalika mashauri mengine yatakayosikilizwa hapo baadaye ni
pamoja na yale ambayo wahusika walipewa nafasi ya kuyamaliza nje ya kamati
lakini wakashindwa.
Post a Comment