KIUNGO wa
Arsenal, Mesut Ozil amesisitiza kwamba atahakikisha anaipata jezi namba 10
ambayo ilikuwa inavaliwa na kiungo wa timu hiyo aliyetolewa kwa mkopo Bournemouth,
Jack Wilshere.
Ozil ambaye
ni raia wa Ujerumani tangu amejiunga na kikosi hicho amekuwa akivaa jezi namba
11 lakini sasa ameona isiwe shida ni vyema akabadili na kuchukua 10 ambayo
kabla ya Wilshere ilikuwa inavalia na Van Persie aliyeihama timu hiyo na
kutimkia United.
Ikiwa
atafanikiwa kuivaa hiyo basi atakuwa ana ‘mechisha’ na ile ya timu ya taifa
ambayo ameichukua ya straika Lucas Podolski aiyestaafu kuichezea timu ya taifa.
"Kwangu
mimi, jezi namba 10 ina maana kubwa sana," Ozil alisema wakati akihojiwa juu ya jezi
namba 10 ya Ujerumani. "Ni namba ninayoipenda kuliko zote. Manguli wa soka
kama Zinedine Zidane, Diego Maradona na Pele wamewahi kuvaa jezi zenye namba
10. Nina furaha sana juu ya jezi hiyo.
"Nilitaka
kuipata jezi hii miaka michache iliyopita, lakini alikuwa akivaa Lukas Podolski
na alikuwa amecheza mechi nyingi zaidi yangu. Lakini sasa nimeipata rasmi.
Alipoulizwa
kama anataka kufanya hivyo na Arsenal pia kuichukua jezi hiyo iliyoachwa na
Wilshere, Ozil alijibu: "Ndio, kwasababu haina mtu, basi naihitaji
sana."
Post a Comment