Mwashiuya fiti sasa mtamkoma
BAADA ya kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu kutokana na majeraha, winga wa Yanga, Godfrey Mwashiuya, ameanza mazoezi mepesi tayari kurejea dimbani kuichezea timu hiyo mechi zijazo, ukiwemo mpambano dhidi ya Simba.
Simba na Yanga zitashuka dimbani katika pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa Oktoba Mosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Yanga, Haruna Ali, alisema jana kuwa Mwashiuya ameanza mazoezi mepesi na baada ya wiki mbili atakuwa fiti na kuendelea na programu za makocha.
“Kwa sasa ameanza mazoezi mepesi na baada ya wiki au mbili atakuwa fiti kabisa, hivyo ataendelea na programu za makocha na wachezaji wenzake,” alisema.
Kurejea kwa Mwashiuya kutaifanya Yanga kuwa imara zaidi katika eneo la winga ambalo pia ina wakali wengine, akiwemo Simon Msuva na Mahadhi Juma.
Post a Comment