Sentahafu wa
Young Africans, Kelvin Yondani si miongoni mwa wachezaji 18 walioondoka leo
Septemba mosi, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya
makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON
2017).
Taarifa
ambazo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipata ni kwamba Yondani
ana matatizo ya kifamilia ambako hajayaweka sawa hadi timu hiyo inaondoka
kwenda Nigeria na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa hajajaza
nafasi hiyo.
Mkwasa amekerwa na kitendo hicho, lakini TFF
itasubiri ripoti ya kocha huyo mara baada ya kurejea kutoka Nigeria.
Timu hiyo
imeondoka na wachezaji 18 huku ikitarajiwa kuungana na na Nahodha wa timu hiyo,
Mbwana Samatta nchini Nigeria. Samatta - Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania
anayechezea timu ya Genk ya Ubelgiji anatokea jijini Brussels ambako makocha
wake wamemwomba Mkwasa na Daktari wa Taifa Stars, Richard Yomba kumwangalia
namna ya kumtumia kwa sababu ya uchovu wa mechi nzito zilizoipa matokeo mazuri
ya kutinga hatua ya makundi ya Uropa Ndogo.
Taifa Stars
inakwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo,
Super Eagles utakaofanyika Septemba 3, 2016.
Licha ya
mchezo huo kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za
AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri
kufuzu kwa fainali hizo kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia
ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji waliosafiri ni:
Makipa-
Said Kipao –
JKT Ruvu
Aishi Manula
– Azam FC
Mabeki
Vicent
Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji
- Young Africans
Mohamed
Hussein – Simba SC
Shomari
Kapombe - Azam FC
David
Mwantika - Azam FC
Viungo
Himid Mao -
Azam FC
Shiza
Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba
– Mtibwa Sugar
Jonas Mkude
– Simba SC
Muzamiru
Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi
- Young Africans
Farid Mussa
Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Jamal Mnyate
– Simba
Simon Msuva
- Young Africans
Ibrahim Ajib
– Simba SC
John Bocco -
Azam FC
Mbwana
Samatta –KRC Genk ya Ubelgiji
Viongozi waliosafiri na timu hiyo ni:
Ahmed Mgoyi
- Mkuu wa msafara
Charles
Boniface Mkwasa- Kocha Mkuu
Hemedi
Morocco – Kocha Msaidizi
Hussein
Swedi – Mtunza Vifaa
Richard
Yomba – Daktari wa timu
Post a Comment