MPAMBANO wa marudiano kati ya bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury's dhidi ya Wladmir Klitscko limethibitishwa kufanyika Oktoba 29 litakalofanyika Ukumbi wa Manchester.

Fury, 28, ambaye ni bingwa wa Uingereza, alishinda mataji ya WBO,WBA, na IBF kutoka kwa Klitscko, 40, raia wa Ukraine Novemba mwaka 2015, lakini akajiondoa katika pigano la marudio lililopangwa kufanyika mwezi Julai kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.

''Ninafurahi kwamba tutapigana tena. Sasa tuwapatia mashabiki kile walichokitaka,” alisema Meneja wa Tyson Fury na mjomba wake Peter.

Klitschko alikuwa hajawahi kushindwa kwa miaka 11 na alimiliki mikanda hiyo tangu mwaka 2006 kabla ya kupoteza kwa Fury mjini Dusseldorf kwa wingi wa pointi.

Post a Comment

 
Top