West Ham United imetangaza
kuachana na mpango wa kutaka kumrudisha klabuni hapo Mshambuliaji wake wa zamani,Muargentina
Carlos Tevez,baada ya staa huyo wa zamani wa vilabu vya Manchester City na
Juventus kutaka apewe mshahara £250,000 kwa wiki ili asaini kuichezea tena
klabu hiyo aliyoinusuru kushuka daraja mwaka 2006-07.
Akitangaza uamuzi huo Mmiliki wa
klabu hiyo, David Sullivan,amesema Westham United ilitaka kumsajili kwa mara
nyingine Tevez,32,lakini kutokana na madai yake ya mshahara kuwa makubwa
wameamua kuachana mpango huo.
Sullivan ameongeza kuwa uwezo wa klabu yake
ulikuwa ni kulimpa Tevez mshahara wa £150,000 kwa wiki pamoja na bonasi nzuri
ambayo ingemfanya awe mchezaji anayelipwa vizuri katika historia ya klabu hiyo.
Kwa sasa Tevez anaichezea klabu ya Boca Juniors ya nyumbani kwao Argentina
baada ya kuachana na Juventus mwaka 2015.
Post a Comment