MOJA ya
tatizo lililochangia jicho moja la Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano
cha Simba, Haji Manara kushindwa kuona ni damu kuganda.
Taarifa
kutoka nchini jijini New Delhi, India zimesema, katika vipimo vya awali
imegundulika damu iliganda ndani ya jicho hilo na kusababisha kushindwa kwenda
katika mzunguko wa kawaida.
“Wamesema tayari wamempa dawa za mwanzo baada
ya vipimo hivyo lakini baada ya hapo kesho (leo), atachukuliwa vipimo zaidi,”
alisema Mtanzania anayeishi jijini Delhi ambaye amekuwa karibu na Manara.
“Tulikwenda kumuona, wametupa taarifa hizo
lakini wamesema matibabu yameanza na wana matumaini makubwa ataweza kuona tena.
Lakini vipimo vingine vitachukuliwa kwa uhakika zaidi.”
Manara
mwenyewe alipatikana baadaye na kusema kweli ameanza matibabu.
“Ninashukuru
kwa kuwa nimeanza matibabu na nimeelezwa mambo mengi sana, hivyo acha nimalize
vipimo vya kesho (leo) halafu ninaweza kuelezea zaidi.
“Lakini
wamesema kuna matumaini ingawa ni tiba inayohitaji uvumilivu kwa kuwa ina mambo
mengi sana,” alisema Manara, jana jioni.
Manara hivi
karibuni aliamka jicho lake likiwa limepoteza uwezo wa kuona na tiba yake
inatarajia kutumika zaidi ya Sh milioni 22.
Post a Comment