MSHAMBULIAJI mpya wa Stand United, Abaslim Chidiebere amesema lengo lake kubwa msimu ujao ni kuhakikisha anafunga mabao 20 kwenye ligi kuu.
Msimu uliopita straika wa Yanga, Amissi Tambwe ndiye aliibuka mfungaji bora baada ya kutupia kambani magoli 21.
Chidiebere amejiunga na Stand United hivi karibuni akitokea Coastal Union ambayo imeshuka daraja baada ya kumaliza mkataba wake.
TAMBWE

Akizungumza  na Spotiripota Chidiebere alisema: “Lengo langu ni kufunga mabao 20 msimu ujao, zaidi nataka kuwa mfungaji bora hivyo siangalii wenzangu watakujaje lakini mimi ninataka kuisaidia Stand imalize ligi ikiwa kwneye nafasi nzuri zaidi.”

Post a Comment

 
Top