HUKU baba yake, Koffi Olomide akiachiwa kwa dhamana baada ya kutakiwa kufungwa miezi kumi na nane jela, mwanamitindo anayechipukia kwa kasi, Didi Olomide ameanza kukimbiza katika fani ya mitindo nchini Ufaransa hali inayomfanya kila mtu kumtabiria mazuri huko mbeleni.

Koffi Olomide raia wa DR Congo, juzi kati alitimuliwa nchini Kenya alikokwenda kwenye shoo kutokana na kusambaa kwa video iliyomuonyesha akimpiga teke dansa wake.


Didi, 16, ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali kwa kuwa na umbo kali kiasi kwamba jarida ‘bab kubwa’ la Vogue liliamua kuzitumia picha zake na kuweka maneno ya kumsifia kutokana na muonekano wake wa umbo, mavazi na nywele.

Watu wengi wamekuwa wakimsifia katika mitandao ya kijamii hasa Instagram na kumtabiria kwamba atakuwa tishio siku za usoni kwani kitendo cha kusifiwa na jarida hilo kimemfanya kukubalika huku yeye mwenyewe akiwa na ndoto za kuwa mmoja wa wanamitindo wanaosimamiwa na mwanamitindo Jean Paul Gaultier.


Post a Comment

 
Top