Baadhi ya waamuzi ambao walichezesha
ligi kuu msimu uliopita
|
WAKATI kesho Jumamosi, waamuzi wa soka
hapa nchini wakitarajia kuanza maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa
kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili, uongozi wa Chama cha Waamuzi Tanzania
(Frat), umelichimba mkwara Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Katika kikao cha Frat cha tathmini ya
msimu uliopita ambacho kilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, uongozi
huo uliitaka TFF kuthamini kazi kubwa inayofanywa na waamuzi, lakini pia
kuwasaidia pindi wanapokumbana na vitendo vya kutishiwa usalama wa maisha yao
wanapokuwa uwanjani.
Hatua hiyo ya Frat imekuja baada
ya TFF kushindwa kuwachukulia hatua kali za kinidhamu baadhi ya viongozi wa
Coastal Union waliowafanyia vitendo vya kinyama waamuzi waliochezesha mechi
namba 77 ya Otoba 31, 2015 kati ya timu hiyo na Mbeya City iliyofanyika kwenye
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Licha ya taarifa zote
zilizotolewa juu ya mchezo huo, hakuna hatua zozote walizochukuliwa viongozi
hao kwa unyama waliofanyiwa waamuzi hao ambapo waliwapiga kwa kushirikiana na
mashabiki wa timu hiyo na kuwapora simu zao za mkononi pamoja na fedha.
Mwenyekiti wa Frat, Nassor Mwalimu,
ameliambia Championi Ijumaa kuwa TFF wanapaswa kulifanyia kazi suala hilo kwa
faida ya maendeleo ya mchezo wa soka hapa nchini lakini pia liwe fundisho kwa
wengine wote wenye tabia hiyo.
Post a Comment