MSAFARA wa watu 30 wa Yanga SC, wakiwemo wachezaji 20 unatarajiwa kuondoka Jumamosi kwenda Ghana tayari kwa mchezo wa marudiano Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Medeama wiki ijayo.
Yanga iliingia kambini leo katika hoteli ya Tiffany, katikati ya jiji la Dar es Salaam kuanza rasmi maandalizi ya mchezo huo huki ikifanya mazoezi Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini.
Yanga watakuwa wageni wa Medeama Jumatano ya Julai 27, mwaka huu Uwanja wa Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi, Ghana.Bournemouth friendly.
Wachezaji Hassan Kessy na Vecent Bossou ni kati ya wachezaji watakaobaki nchini hapa. Kessy bado anashughulikia ishu yake na Simba na Bossou yeye ana kadi za njano hivyo hatacheza mchezo ujao.

Post a Comment

 
Top