Katika hatua nyingine, Tambwe amesema kuwa Yanga imelamba dume kwa kufanikiwa kumsajili Andrew Vincent, aliyedai kuwa ni mchezaji mzuri mno, iwapo ataaminiwa na kupewa nafasi zaidi.
Tambwe alisema kwamba, beki huyo mpya wa kati anaweza kuwa msaada mkubwa katika ukuta wa kikosi chao.
Ukuta wa Yanga ambao unaundwa na Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Oscar Joshua, Pato Ngonyani na Mwinyi Haji, umeonekana kuruhusu mabao ya kizembe katika mechi zake za kimataifa.
Vicent ambaye aliingia kipindi cha pili kwenye mchezo kati ya Yanga na Medeama uliopigwa wiki iliyopita ugenini na Wanajangwani hao kufungwa mabao 3-1, kwa kiasi kikubwa aliweza kuwadhibiti washambuliaji wa wapinzani wao hao na kupunguza kasi yao.
Dante wa kwanza kushoto
“Tuna tatizo katika beki ya kati, lakini Vincent anaweza kuwa msaada mkubwa kwetu, alicheza vizuri sana alipoingia, utaona hata kipindi cha pili hatukuweza kuruhusu mabao ya kizembe kama kipindi cha kwanza,” alisema Tambwe.
Alisema Vicent alicheza vizuri pamoja na Cannavaro baada ya kutolewa kwa Yondani kipindi cha pili.

Post a Comment

 
Top