WACHEZAJI wa Yanga wameipongeza ratiba ya Ligi Kuu
Bara msimu ujao ambayo imetolewa hivi karibuni na Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) ila wameenda mbali kidogo kwa kusema; “Kwa jinsi tunavyoiona basi ubingwa
ni wetu tena.”
Wamedai
kuwa watani zao Simba na Azam FC wajipange kuwania ubingwa wa Kombe la FA ili
waweze kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa lakini kuhusu ubingwa
wa ligi kuu wasahau.
Kwa
mujibu wa ratiba hiyo, ligi kuu itaanza Agosti 20, mwaka huu ikitanguliwa na
mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 17, kati ya Yanga na Azam.
Kiungo
wa Yanga, Haruna Niyonzima alisema: “Nimeiona ratiba hiyo, ni nzuri kwa kiasi
chake ukilinganisha na ile iliyopita, ni matumaini yangu tunaweza kutetea
ubingwa wetu kama TFF wasipoivuruga.”
Kwa
upande wake, Amissi Tambwe alisema: “Ratiba nimeiona na imepangwa vizuri kwani
zaidi ya mechi zetu tano za mwisho tutacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani.”
“Msimu
uliopita idadi ya mechi kama hizo tulicheza ugenini tena mfululizo bila ya kupumzika,
endapo Mungu atakuwa nasi na ratiba isipovurugwa, tutatetea tena ubingwa wetu,”
alisema Tambwe.
Post a Comment