JUZI Jumatatu Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der
Pluijm aliukabidhi uongozi wa timu hiyo ripoti yake ya mechi ya kimataifa ya
kuwania Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana iliyofanyika
Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ripoti hiyo imedaiwa kuushtua uongozi wa timu hiyo kutokana
na mambo mbalimbali ambayo kocha huyo ameyaainisha ndani yake yanayohusiana na
mechi hiyo ambayo Yanga ilitoka sare ya bao 1-1.
Moja ya mambo makubwa yaliyoushtua uongozi wa timu hiyo ni jinsi
kocha huyo alivyosema kuwa kuwa wachezaji wake waliachana na maagizo yake na
kuamua kucheza wanavyojua wao.
“Ukiachana na hilo pia yapo mambo mengine ambayo pia
ameyaainisha ambayo kimsingi siyo vizuri kuyasema lakini kwa namna moja ama
nyingine uongozi utakuwa umeyaona na utayafanyia kazi.
“Siyo ripoti nzuri kwa kuwa imeonyesha jinsi hali ilivyo,”
kilisema chanzo hicho cha habari.
Alipouliza kuhusiana na suala hilo Katibu Mkuu wa Yanga,
Baraka Deusdedit alisema kuwa: “Ni kweli kabisa ripoti hiyo tumeshaipokea na
kuna mambo mengi ambayo kocha ameyaainisha na siyo vizuri kuyaweka wazi lakini
jambo kubwa na la msingi ambalo naweza kusema ni kwamba tutaifanyia kazi
ipasavyo.
“Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika
mechi zetu zilizobaki hivyo tunamshukuru kocha kwa ripoti yake hiyo na sisi
kama uongozi tutayafanyika kazi yale yote yanayotuhusu,” alisema Baraka.
Post a Comment