Kipa
Mhispania kulia |
UONGOZI wa Azam FC umetangaza kuachana na kipa Mhispania,
Juan Jesus Gonzalez na kumpa mkataba wa mwaka mmoja kipa Muivory Coast, Daniel
Yeboah.
Gonzalez na Yeboah wote walikuwa wakifanya majaribio na
kikosi hicho chini ya makocha wa Kihispania wakiongozwa na kocha mkuu, Zeben
Hernandez.
Ofisa habari wa timu hiyo, Jafar Idd, amesema benchi la
ufundi limeridhishwa na kiwango cha Yeboah, likaamua kumpa mkataba wa mwaka
mmoja na kuachana na Gonzalez kwani kati ya makipa hao wawili, kulikuwa na
nafasi moja waliyokuwa wakiipigania.
“Tayari yule, Mhispania ameshaondoka na kurudi kwao baada ya
kukosa nafasi.
“Pia Jumamosi tunatarajia kucheza na KMC ikiwa ni muendelezo
wa kukipima kikosi chetu,” alisema Idd.
Post a Comment