KOCHA Mkuu wa Klabu ya
Mwadui ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amefumba macho na kuamua kuwatema
wachezaji wakongwe wakiwemo Jerry Tegete na Athuman Idd ‘Chuji’ waliowahi
kuichezea Yanga.
Julio amesema amefanya
uamuzi huo ili kuingiza changamoto mpya katika kikosi chake.
Wachezaji wengine ambao Julio
amewatema katika kikosi chake ni ndugu Nizar na Razak Khalfan pamoja na Kelvin
Sabato ‘Kiduku’ ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora wakati Mwadui ilipopanda
daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2014-15.
Julio ambaye amewahi kuinoa Simba, amesema
hajutii kuwaacha wachezaji hao wakongwe kwenye kikosi chake kutokana na kutaka
kuingiza changamoto mpya.
“Hatuna wasiwasi wa kutamba kwenye
msimu ujao kwa sababu tumefanya usajili makini na wachezaji wote wana viwango
vikubwa ambapo naamini wataziba vizuri kabisa mapengo ambayo yameachwa na
wachezaji niliowaacha msimu huu,” alisema Julio.
Mwadui tayari imeshawanasa wachezaji
Miraji Athuman ‘Shevchenko’ na Abdallah Seseme wote wa Toto, Salum Kanoni
aliyekuwa Kagera Sugar na Masoud Nassor ‘Chollo’ aliyekuwa Stand United.
Tegete amesema kuwa yupo katika
mazungumzo na African Lyon ili ajiunge nayo.
CHANZO: Championi
Post a Comment