goma, lakini nyota wa Simba, Ibrahim Ajib amemcheki straika anayesubiri kusajiliwa katika timu hiyo, Fredric Blagnon raia wa Ivory Coast jinsi anavyopiga chenga, anavyofunga kisha akasema: “Jamaa balaa.
Ajib ameenda mbali kwa kusema: “Kama huyu jamaa (Blagnon) akisajiliwa, tutakuwa tumepata straika mkali atakayetusaidia katika Ligi Kuu Bara.”
Ngoma, raia wa Zimbabwe, amekuwa msaada mkubwa kwa Yanga msimu uliopita wa ligi kuu na hata sasa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakitambia uwepo wake.

Ajib alisema Blagnon ni mtu anayefahamu mpira unataka nini, lakini pia anajua umuhimu wake kikosini, hivyo hafanyi makosa anapopata nafasi.
“Mabao mawili aliyofunga na kiwango alichoonyesha katika mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Moro (Simba ilishinda mabao 6-0), kimeonyesha jamaa anaweza kutusaidia.
“Namuona anafaa, hata tunapokuwa naye mazoezini na hata katika ile mechi ya Polisi alicheza vizuri, anajua afanye kitu gani wakati upi,” alisema Ajib, mfungaji wa Bao Bora la Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Blagnon aliyewahi kuichezea Asante Kotoko ya Ghana, alitua nchini kufanya majaribio Simba wiki nne zilizopita. Wengine wanaoendelea na majaribio Simba ni beki Mzimbabwe, Method Mwanjali na Wacongo, Mussa Ndusha na Besala Bokungu.


Post a Comment

 
Top