Mchezaji mmoja raia wa Nigeria
ametibua mipango ya straika wa zamani wa Azam, Didier Kavumbagu kujiunga na
timu moja ya Vietnam.
Kavumbagu alifanya majaribio na
timu ya Dong Tan akafuzu, akaomba Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lakini wakati hati yake inafika kwa timu
hiyo, jamaa wakawa wamebadili maamuzi kwa kumchukua Mnigeria, ndipo akapelekwa
kufanya majaribio timu nyingine ambayo ilimkubali lakini kikwazo kikawa ni ITC
ambayo inashikiliwa na Dong Tan na kanuni za Fifa zinasema ni mpaka mchezaji
awe amecheza mwaka mmoja ndiyo anaweza kupata ITC nyingine.
Kavumbagu alisema: “Nilifanya
majaribio katika timu ya Dong Tan nikafuzu, ajabu wakamsajili mchezaji kutoka
Nigeria, nami nikaenda timu nyingine. Sasa Dong walikuwa wameshapewa ITC yangu.
“Ikaonekana kama nimesajili timu
mbili lakini haikuwa hivyo, meneja wangu alikasirika sana ila Dong nao wanaona
kama wametumia fedha zao bure kwangu, ila mambo yanaenda sawa naweza kucheza
Oktoba ligi mpya itakapoanza.”
Post a Comment