KOCHA msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja ametamka
kuwa klabu hiyo itaendelea na kambi za kujificha kwa ajili ya kukwepa mbinu zao
kuigwa na wapinzani wao ikiwemo Yanga jambo ambalo linaweza kuathiri kiwango
chao.
Mayanja pamoja na kocha mkuu wa kikosi hicho cha Simba,
Joseph Omog wamejichimbia mkoani Morogoro kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na
msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mayanja ambaye ni kocha wa zamani wa Coastal Union na Kagera
Sugar amesema kuwa, wataendelea kufanya kambi yao kwa usiri mkubwa kwa kuwa
hawataki wapinzani wao wafahamu juu ya kile ambacho wanakifanya ikiwa ni pamoja
na namna wanavyojiandaa.
“Tunataka tufanye vizuri kwenye msimu ujao hivyo ni lazima
kutoweka wazi kila kitu ambacho tutakuwa tunakifanya kama ambavyo tumejichimbia
huku kwa ajili ya kuficha mbinu ambazo tutazitumia kwa msimu ujao.
“Unajua kuwa mpinzani wako akikujua jinsi ulivyo inakuwa ni
rahisi kwake kukukabili sasa sisi hilo hatutaki litokee na ndiyo maana
tunayafanya mambo yetu kwa usiri mkubwa kwa ajili ya kuwafanya maadui zetu
wakiwemo wapinzani wetu Yanga wasijue kile tunachokifanya,”alisema Mayanja.
Post a Comment