BAADA ya kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko raia wa Zimbabwe
kupata tuzo ya mchezaji bora wa kigeni katika tuzo zilizotolewa na Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) juzi , mchezaji huyo ametangaza vita katika msimu ujao
wa ligi kuu.
Kamusoko aliibuka kinara wa mchezaji bora wa kigeni kwa
kupata zawadi ya sh milioni 5, huku akiwapiku Donald Ngoma raia wa Zimbabwe
pamoja na Vicent Angban wa Simba raia wa Ivory Coast.
Akizungumza jijini Dar, Kamusoko alisema anashukuru kwa
ushirikiano alioupata msimu uliopita hadi kufikia kupata tuzo hiyo ya mchezaji
bora wa kigeni, hivyo kwa sasa nguvu zake anazielekeza katika msimu ujao ili
aweze kufanya vizuri zaidi.
“Nachukua nafasi hii kuwashukuru watu wote walionipa
ushirikiano msimu uliopita, kwani ulikuwa ni msimu mzuri kwangu na timu yangu
ya Yanga kwa ujumla kwa ushirikiano walionipa.
“Pia nawashukuru wadhamini ambao ni Vodacom kwa kunichagua
mimi kuwa mchezaji bora wa kigeni na
bila ya kuwasahau wote walionipa ushirikiano ndani ya Yanga, hivyo kwa
sasa mtazamo wangu ni katika msimu ujao
ili nifanye vizuri,” alisema Kamusoko.
Ukiachana na Kamusoko wachezaji wengine waliopata tuzo katika
kikosi cha Yanga ni pamoja na Amissi Tambwe ambaye alitwaa tuzo ya mfungaji
bora wa msimu, Juma Abdul aliyepata tuzo ya mchezaji bora wa msimu pamoja na
kocha wao Hans van Pluijm aliyepata tuzo ya kocha bora.
Post a Comment