MENEJA wa sasa
wa Klabu ya Sunderland, Sam Allardyce anatarajiwa kuthibitishwa kuwa meneja mpya
wa Timu ya Taifa ya England .
Bodi ya
Chama cha Soka England, kitakaa kumpitisha kama meneja wao mpya kuchukua nafasi
ya Roy Hodgson aliyemaliza mkataba wake hivi karibuni baada ya kuisha kwa
Michuano ya Euro 2016, na England kutolewa kwenye hatua ya mtoano na Iceland.
Kwenye
mchakato wa uteuzi wa wadhifa huu, Allardyce, maarufu kama Big Sam, alichuana
vikali na Meneja wa Hull City Steve Bruce aliyewahi kuichezea Manchester
United.
Mtendaji
Mkuu wa FA, Martin Glenn, alithibitisha kuwa Bodi ya Watu 12 ya FA itajulishwa
rasmi kuhusu mchakato wa uteuzi wa Meneja wa timu ya taifa ili itoe uamuzi
kwenye kikao chao cha leo Alhamisi.
Waliopewa
mamlaka ya kupendekeza nani atakuwa Mrithi wa Roy Hodgson ni Glenn mwenyewe,
Makamu Mwenyekiti wa FA, David Gill, aliewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Man United,
na Mkurugenzi wa Ufundi, Dan Ashworth.
Aliewahi
kuwa Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson aliwaeleza wazi viongozi wa FA kuwa
mtu pekee anayefaa wadhifa wa kuwa meneja wa England ni Sam Allardyce ‘Big Sam’.
Post a Comment