ALIYEKUWA nahodha wa Simba,
Hassan Isihaka, ametamka kuwa kwa sasa hana timu ya kuichezea na yupo nyumbani
tu.
Isihaka ambaye alitengeneza
ukuta imara akiwa Simba akishirikiana na Mganda, Juuko Murshid, ametemwa nje ya
kikosi cha Simba ambacho kimejichimbia mkoani Morogoro chini ya kocha wake
Mcameroon, Joseph Omog kikijiandaa na msimu ujao wa ligi kuu.
Nahodha huyo alisema kuwa
mpaka sasa amekuwa akikaa nyumbani tu kutokana na kutemwa na timu yake hiyo
ambapo hakuna timu yoyote ile iliyomfuata kwa nia ya kumsajili.
“Nipo nyumbani tu, sina timu
yoyote ya kuichezea mara baada ya kutemwa na Simba ambapo mpaka sasa hakuna
timu yoyote ile ambayo imenifuata kwa ajili ya kunisajili kwa msimu ujao.
“Sijajua hatma yangu
itakuwaje msimu ujao kwa sababu sina timu lakini naamini mambo yatakuja kukaa
vizuri kabla ya dirisha la usajili kufungwa, timu zitakuja tu,” alisema
Isihaka.
Post a Comment