Waamuzi waliochezesha mchezo wa Yanga
na Medeama, Taifa.
|
Tayari majina ya waamuzi wa mchezo wa
marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika wa Yanga dhidi ya Medeama ya Ghana
yameshawekwa wazi na kwa mara nyingine baada ya mchezo wa awali wa jijini Dar
kuamuliwa na Wamisri, safari hii utaamuliwa na Wamorocco.
Majina hayo yamewekwa juzi na Mtandao
wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ambapo mwamuzi wa kati atakuwa RĂ©douane
Jiyed akisaidiana na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou.
Wachezaji wa Medeama
wakishangilia goli.
|
Jihed mwenye miaka 36, atachezesha
mchezo huo mgumu utakaopigwa kesho Jumanne katika Uwanja wa Essipong Sports
jijini Sekondi, Ghana ambapo kila timu itahitaji ushindi wake wa kwanza baada
ya michezo yao mitatu ya awali kutopata matokeo ya kuridhisha.
Katika mchezo wa awali uliopigwa Dar,
Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Yanga kubaki mkiani mwa Kundi A baada ya
kufungwa katika michezo mingine miwili ya awali. Medeama ipo nafasi ya tatu,
imefungwa mechi moja na kutoa sare mbili.
Yanga ina pointi moja, Medeama ina
mbili, MO Bejaia ya Algeria inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tano,
vinara TP Mazembe ya DR Congo wamekusanya pointi saba mpaka sasa
Post a Comment