RAIS wa zamani wa Barcelona, Joan
Laporta amesema klabu hiyo haimthamini nyota wake Lionel Messi licha ya
mafanikio aliyonayo.
Laporta alisema tangu alipoondoka
madarakani Messi amekuwa hathaminiwi ndani ya uwanja na rais mpya wa timu hiyo,
Josep Maria Bartomeu amedangaya mambo mengi.
Wakati wake tangu alipoingia
madarakani mwaka 2003, Laporta alifanikiwa kuiimarisha Barcelona kwa majengo na
matokeo mazuri uwanjani kuliko kipindi chochote.
Laporta ameonyesha wazi kutopendezwa
na uongozi wa Bartomeu akisisitiza kuwa, unatakiwa kufanya kitu cha ziada ili
kuendeleza kipaji cha Messi.
"Klabu haipo katika kiwango cha Messi,"
alisema Laporta na kuongeza: "Huyu ni mchezaji bora wa kihistoria, ni
mchezaji bora wa dunia."
Laporta alisisitiza kwamba, Bartomeu aliahidi vitu vingi katika kampeni
zake mwaka jana lakini vingi hajatimiza hadi leo.
Post a Comment