SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limetoa madawati 200 ikiwa ni sehemu ya mapato ya Ngao ya Hisani utakaochezwa
Agosti 17, 2016.
TFF inaunga
mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na juhudi za Serikali
kwa ujumla katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa na mazingira bora
ya kupata elimu.
Kadhalika
TFF inamshukuru Katibu Mkuu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah kwa juhudi za
kuendelezaa mpira wa miguu na kuutumia katika kuliletea Taifa maendeleo.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania litaendelea kushirikiana na Ofisi ya Bunge Sports
Club katika kufanikisha mashindano mbalimbali hasa mhezo wa Hisani kati ya
Simba Sports Club na Young African (Wabunge) utakaofanyika hapo baadaye kwa
mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.
Post a Comment