KLABU ya Simba imeripotiwa kuendelea na mchakato wake wa usajili na sasa wanataka kuhakikisha wanakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Azam FC, Mae Ali ‘Zungu’.
Ame Ali amebakiza msimu mmoja tu wa kuitumikia Azam amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo tangu alipojiunga nayo akitokea Mtibwa Sugar ambako alikuwa anacheka na nyavu mara kwa mara.

Chanzo kutoka Simba kinadai kuna uwezekano mkubwa Zungu akajiunga na kikosi hicho kilichoweka kambi mjini Morogoro ndani ya siku tatu zijazo mara baada ya kukamilisha usajili.
Simba sasa inahaha kutafuta straika atakayeziba pengo la Hamis Kiiza ambaye ameachwa licha ya kuwa mfungaji bora kwenye kikosi hicho msimu uliopita akiwa katupia nyavuni mabao 17 kwenye ligi kuu.

Post a Comment

 
Top