Liverpool, England
SIRI za kambi ya timu ya Liverpool kwenye hoteli yao imevuja na kuelezwa mambo mbalimbali wanayotaka mastaa wa kikosi hicho cha Anfield kinachonolewa na Jurgen Klopp.
Wakati Liverpool ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu England sambamba na kucheza mechi kibao za kirafiki, kwenye hoteli waliyofikia nyota wake wametoa masharti ambayo sasa yamevuja na kufahamika kwenye mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa matakwa ya kushangaza waliyotaka wachezaji wa Liverpool kwenye hoteli waliyoweka kambi, kwamba nahodha wa kikosi, Jordan Henderson ametaka chumba chake kiwe karibu na Adam Lallana, wakati kocha Klopp ni lazima apewe chumba chenye hadhi kubwa ambacho kinaruhusu kuvuta sigara na moshi usiendelee kubaki chumbani kwa muda mrefu.
Philippe Coutinho chumba chake kisiwe na kipoza hewa bali kiwa na feni na kwamba vilevi vyote pamoja na vitu vya kutafunatafuna viondolewe kwenye vyumba vya wachezaji. 

Matakwa ya wachezaji hao yote yamewekwa kwenye video moja ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kikosi cha Liverpool kwa sasa kipo Marekani ambako kitacheza mechi na Chelsea, AC Milan na AS Roma.

Post a Comment

 
Top