KIKOSI cha Azam FC ya Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar, jana kimemaliza vyema ziara yake visiwani Zanzibar baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Taifa Jang’ombe, ukiwa ni mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani humo ukiwa ni wa pili, bao pekee la Azam lilifungwa na mchezaji aliye kwenye majaribio aitwaye Khamis Mcha aliyetupia dakika ya tano. Leo Jumapili Azam wanatarajiwa kutua Dar.
Kikosi Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Bruce Kangwa/Gadiel Michael dk 46, David Mwantika/Ismail Gambo dk 46, Aggrey Morris, Jean Mugiraneza, Himid Mao/Masoud Abdallah dk 46, Michael Bolou/Mudathir Yahya dk 46, Frank Domayo/Salum Abubakar dk 46, Khamis Mcha/Fuadi Ndayisenga dk 46, John Bocco (C)/Ibrahima Fofana dk 46, Ramadhan Singano/Brian Abbas dk 46.

Post a Comment

 
Top