RIO DE JANEIRO, Brazil
HUENDA ikawa auheni kwa wanamichezo
watakaoshiriki Michezo ya Olimpiki mwaka huu kwani kondomu 45,000 zitagawiwa
bure kwa washiriki ili kujikinga na magonjwa mbalimbali.
Kondomu hizo zitawekwa katika maeneo
mbalimbali ya kijiji cha Olimpiki ambapo wanamichezo watazipata kwa urahisi na
kuzitumia kujikinga.
"Sherehekea na kondomu.” ndivyo
inavyosomeka kauli mbiu ya kusisitiza matumizi ya kondomu hizo iliyowekwa na
waandaaji.
Kutakuwa na mashine maalumu 40 ambazo
zitawekwa kondomu ndani yake na mtumiaji anaweza kuchukua kirahisi na kuzitumia
katika kijiji hicho cha Olimpiki.
Kwa mujibu wa takwimu, kondomu hizo 450,000
ni rekodi ya kipekee katika Olimpiki ikiwa ni mara tatu zaidi ya zile
zilizotumika katika Michezo ya Olimpiki iliyopita 2012 jijini London.
Pia kampeni hiyo inaendeshwa ili
wanamichezo pia kujikinga na virusi vya ugonjwa hatari wa Zika.
Post a Comment