Mlinzi wa kati Rajabu
Zahir aliyekuwa akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Stand United
akitokea Dar Young Africans ya jijini
Dar es Salaam amejiunga na kikosi cha
Mbeya City Fc leo.
Kwenye ofisi za City zilizopo Mkapa Hall, eneo la Soko
Matolla, jijini hapa, Zahir, amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kujunga na kikosi cha kocha Kinnah phiri na kusema kuwa ana imani kubwa ya kupata
mafanikio yake kisoka akiwa na chini ya
kocha huyo bora
kutoka Malawi.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kujiunga na City, hii ni
moja kati ya timu kubwa nchini kwa sababu ina ushawishi wa kutosha kwenye soka la nchini yetu, kitu muhimu ni
kuomba ushirikiano kutoka kwa pande zote
kwa maana ya uongozi wachezaji wenzangu na mashabiki, hayo yote
yatatufanya kutimiza malengo kwa sababu
kila mmoja anahitaji mafanikio katika kazi kwangu mimi hapa ndiyo sehemu ambayo nitayapata” alisema.
Zahir amejiunga na City baada ya msimu mmoja wa mkopo kwa
Stand United ya Shinyanga
uliohitimisha kandarasi yake ya miaka 3 na kikosi cha Yanga ya Dar es Salaam,
Akiwa Stand United, Zahir alifanikiwa kucheza michezo 23
katika mechi zote 30 zilizochezwa na timu hiyo ya Shinyanga na kufanikiwa
kushika nafasi ya 7 ikikusanya jumla ya pointi 40 mwisho wa msimu uliopita.
Post a Comment