TAARIFA
kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa zinasema klabu ya Manchester
United imekubali kutoa dau la rekodi la £100m ili kumsajili kiungo wake wa
zamani,Paul Labile Pogba, ambaye kwa sasa anachezea Juventus.
Makubaliano
ya dili hilo yamefikisha Jumatano usiku kufuatia mwenyeji wa Manchester
United,Ed Woodward,kufanya mazungumzo mazito na Wakurugenzi wa
Juventus,Giuseppe Marotta na Fabio Paratici, pamoja na Wakala wa Pogba
anayeitwa Mino Raiola.
Taarifa
zaidi zinasema ikiwa kila kitu kitakwenda sawa Pogba mwenye umri wa miaka 23
atasaini mkataba mnono wa miaka mitano utakaomwezesha kuvuna mshahara wa
£210,000 kwa wiki na kuwa mmoja kati ya nyota wanaolipwa vizuri England.
Pogba
aliiacha Manchester United mwaka 2012 na kutimkia Juventus akiwa mchezaji huru
baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza ambacho wakati huo
kilikuwa chini Sir Alex Ferguson.
Post a Comment